Ni kisa ambacho kimetokea katika kijiji cha Chepkoilel, kata ndogo ya Seregeya wilaya ya Likuyani kimewaacha wakaazi vinywa wazi.
Imeripotiwa kwamba, mtoto huyo, kwa jina Washington Omollo alivamiwa na mshukiwa kwa jina Allan, alipokuwa anachunga ng'ombe wa nyanyake.
Chifu wa kata ya Likuyani Charles Banda amekikashifu na kukilaani vikali kitendo hicho ambacho alikitaja kama cha kihayawani.
Kulingana na nyanyake mtoto huyo, Hellen Adira, mtoto huyo ana matatizo ya kiakili ambayo amekuwa nayo tangu kuzaliwa.
Mshukiwa amekamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Turbo na atafikishwa mahakamani punde.
Huku hayo yakijiri, kaka wawili wamepigana na kujeruhiana vibaya katika kijiji cha Eluhobe, huko Maseno baada ya kile kimetambulika kama mzozo wa ardhi.