Mkuu wa madaktari kwenye hospitali ya wilaya mjini
Webuye, amempongeza gavana wa kaunti ya Bungoma Kenneth Lusaka kwa juhudi zake
za kuinua viwango vya afya kwenye kaunti hiyo.
Akizungumza afisini
mwake mapema hii leo, daktari Isaac Omeri amesema kuwa serikali ya kaunti imetia
fora kuona kuwa afya inapewa kipaumbele, na akamuomba gavana Lusaka kuendeleza
juhudi hizo.
Hata hivyo, Omeri amesema kuwa fedha zinazopeanwa kwa sekta
ya afya katika kaunti hiyo ni chache, na kuwa haziwezi kuiendesha sekta hiyo
kikamilifu huku akisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikitegemea pesa zinazokusanywa kutoka kwa wagonjwa ambazo pia hazitoshi.
Vilevile daktari huyo ameomba uongozi wa kaunti hiyo ya
Bungoma kutafuta mbinu mbadala za kupata fedha, na kutotegemea serikali ya kitaifa ili
kukuza sekta muhimu kwenye kaunti hiyo.
No comments:
Post a Comment