Dereva wa matatu iliyohusika kwenye ajali ya
barabara na kusababisha vifo vya watu tisa eneo la Kipkaren mwezi mmoja
uliopita ametozwa faini ya shilingi elfu thelathini pesa taslimu na mahakama ya
Webuye.
Akitoa umamuzi huo hakimu mkaazi wa Webuye Stella
Nabwire amesema kuwa mshukiwa huyo kwa jina Vincent Matayo amekiri madai ya
kuendesha gari kwa kasi na kukiuka sheria za barabara huku akionywa dhidi ya
kurudia kosa hilo na kuwa atapokonywa leseni hiyo ikiwa atahusika kwenye ajali
nyingine chini ya miezi sita ijayo.
Nabwire ameitaka mamlaka ya kitaifa ya uchukuzi NTSA
kushirikiana na idara ya trafiki kuwahamasisha madereva na wananchi kuhusu
umuhimu wa kuzingatia sheria za trafiki ili kupunguza visa vya ajali za
barabarani.
No comments:
Post a Comment